BODI ya Pamba Tanzania imesambaza mbegu bora za pamba mkoa wa Pwani kwa lengo la kufufua zao hilo
Afisa Usimamizi wa Bodi ya Pamba Emmanuel Mangulumba alisema hayo wakati Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba ilipokuwa ikiwahamasisha wakulima namna ya kupata pembejeo kwa kutumia mfumo wa vocha.
Mangulumba alisema kuwa Bodi ya pamba imepeleka mbegu bora za pamba kwenye vijiji vilivyoko wilaya ya Bagamoyo na Kibaha.
Mangulumba alisema kuwa wilaya ya Kibaha imepata tani moja ya mbegu bora za pamba kwa ajili ya kijiji cha Magindu, Bagamoyo tani 12 kwa ajili ya wakulima wa vijiji vya kata Kibundu, Mbwewe na Miono
Mangulumba alisema kuwa katika wilaya ya Kisarawe hazikupelekwa mbegu kufuatia uamuzi wa baraza la madiwani kukataa zao la pamba.
Mangulumba alisema kuwa serikali itachangia asiliamia 50 ya bei ya soko ya mbegu bora za pamba na madawa.
Mangulumba alisema kuwa kila ekari moja ya pamba itapata ruzuku ya mbegu ambazo ni kilo 10 za mbegu bora ya pamba kwa ekari.
Tuesday, February 2, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment