Katika uzalishaji na kukuza uchumi ni muhimu kuzingatia muda
Hii inatokana nakuwa bila muda hakuna uzalishaji
Uzalishaji usiojali muda hauna faida wala hautakuwa endelevu, ni lazima kuangalia miundombinu hasa ya barabara
Nalisema hili kwa kuwa ni muda mrefu hapa DSM kumekuwa na miundombinu mibovu kiasi ya kwamba wazalishaji kukaa bararani zaidi ya masaa mawili kutokana na foleni
Mfano barabara ya Mandela ambayo ina zaidi ya miaka miwili sasa tangia ianze kutengenezwa, imekuwa kero kwa kusababisha foleni kwa muda wa miaka miwili sasa
Barabara mategenezo hayaishi na hayana mpangilio matengenezoyasiokuwa na mpangilio … hii inatia huruma japo wakati mwingine inatia hasira
Barabara hii huwezi kujua kuwa wakandarasi walianzia wapi kutengeneza na wataishia wapi kwa kuwa kila siku wanatengeza kipande na kabala hakijaisha wanahamia kungine
Hii inasababisha foleni kubwa ,watu wanachelewa makazini wafanyabiashara wa dadalala ndio kabisa hasara mafuta huishia njini
Hivi serikali wao wapiti njia hii ya Mandela wakaona ?
Sasa kama mfanyakazi anatakiwa kufika kazini saa 1:30 lakin kutokana na foleni akafika saa 3:00 hapo kutakuwa na uzalishaji gani wenye tija ?
Wahusika wa barabara hii mnaombwa kuangalia swala hili.
Wednesday, February 24, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment