Monday, February 8, 2010

uhuru wa habari

Huwa watu wanasema kuwa Uhuru wa vyombo vya Habari ni chimbuko la Demokrasia

Kwa maana kuwa bila uhuru wa kujieleza haitawezekana kuibulia na kufahamu yale mazuri na mabaya (ufisadi) yanayofanywa na viongozi wetu ,

Hayo yanaweza kufanyika tu kama mtu atapata uhuru wa kuongea ambayo ndio Demokrasia

Demokrasia na ufisidi ni sawa na maji na moto ambavyo ki msingi kamwe havikai sehemu moja

Pia ufisadi na uhuru wa habari ni sawa na mwanamke na mwanaume ambao huwa hawafanani japo mmoja anaweza kumuendeleza mwingine

Fisadi huogopa vyombo vya habari kama ukoma kwa maana huweza kumjenga au kumbomoa japo kama waandishi wakiyumba kidogo huweza kulelewa na mafisadi

Katika mazingira ya hivi karibuni jinsi vyombo vya habari vilivyochangia katika vita dhidi ya mafisadi
Swala hili lilileta hofu kwa wale waliokuwa wanafikiri kuwa mafisadi wa kesho au wa leo lakini hawajakomaa

Hii isije kujenga tabaka kati ya wanahabari naumoja wa wanaofikiri kuwa ni mafisadi na kuleta mitikisiko na kutika nguzo hii ya nne ya serikali yaani HABARI

No comments:

Post a Comment