Sunday, November 15, 2009

HUDUMA ZA AFYA ZIBORESHWE HASA KATIKA VITUO HIVI

Tunapozungumzia huduma za jamii tunazungumzia mashule, hospitali barabara na vyombo vya usalama

Na ukiweza kuvitimiza hivyo kwa wakati wake ndio mwanzo wa maendeleo na kama kimoja kitayumba ni wazi kuwa hakuta kuwa na maendeleo

Kwa Tanznia serikali inajitahidi kuwafikishia wananchi huduma hizi kwa ukaribu sana ili kuwasogezea maendeleo karibu zaidi

Lakini hivi itakuwa na maana gani kama kutawa na majengo lakini pasiwepo na vifaa vinanyotarajiwa kuwepo ? mfano shule ili iwe shule ni lazima iwe na vifaa vya kufundishaia pamoja na walimu wa kutosha

Na kwa upande wa hospitali kuwe na mahabara vipimo vya kutoosha na madawa ya kutosha tofauti na hayo hiyo basi sio huduma

Ipo hospitali moja ya serika iliopo Tabata Segerea ambayo kimsingi ni nzuri na ni mpya kwa maana ndio imefunguliwa lakini pia tunaamini kuwa labda hata wafanyakazi wake ni wazuri .

hii inatoka na ukweli kuwa kitu kipya hata mambo yake ni mapya hivyo watu kukimbilia wakijua watapata yalio bora

Lakini swala la kushangaza hata kama una kila dalili ya ya maleria ambayo kila mtu wa kawaida anaweza kuiona lakini wakikupima wanakuambaia eti huna maleria

Lakini ukipima maleria hiyo katika vituo vingine vya afya utakutwa na wadudu kibao wa maleria

Swala hili limekuwa la kawaida sana katika hospitali ile ambapo kama hawatajali hawatakuwa na wadau lakini pia wanaweza kuhusika na matatizo endapo yatatokea

Lakini kwa ukweli hivi vipimo havisomi ukweli au vipimo vimeharibika au hakuana watu wenye uwezo wa kutumia mashine hizo hivyo wanashindwa kuvisoma ?

Maswali mengi kamahaya yamekuwa yakiulizwa na weatua wengi sana na si zani yupo ambaye emepata majibu

No comments:

Post a Comment