Na Bashiri Salum
Watu husema umaskini ni sawa na mzigo wa mzoga ambao kama hutautua kwa ajili ya harufu yake basi utautua kwa uzito wake.
Haya ndio yanayowakuta watu wa Kilimanjaro ambao wana rasilimali ambazo hawazitumii.
Mkoa wa Kilimanjaro unatakiwa kutumia mbinu za ziada ili kuutua mzigo wa upungufu wa chakula unaoikabili mara kwa mara.
Upungufu wa chakula unao ukumba mkoa wa Kilimanjaro unaweza kuzuiliwa kwa kuboresha kilimo, ufugaji na kuanzisha vyama vya akiba na mikopo.
Kutokana na kutegemea mvua za msimu wakulima mkoani Kilimanjaro wamekuwa wakishindwa kupata mavuno ya kutosha kutokana na uhaba wa mvua.
Wakulima wadogowadogo inafaa wawe wanatafuta pembejeo za kilimo kulingana misimu waliyonayo mkoani Kilimanjaro.
Naibu waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh Christopher Chiza alisema kuwa
kilimo cha umwagiliaji ni moja ya mikakati itakoayowezesha mkoa wa Kilimanjaro kuepukana na njaa
Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa chakula , Bi Sophia Kaduma wakati wa mdahalo wa kampeni dhidi ya njaa alisema kuwa mikakati shirikishi inaandaliwa ili kusaidia mikoa hiyo hasa Mikoa ya Kilimanjaro na Singida ilyokumbwa na ukame
Mbali ya ushirikishwaji wa wananchi katika kilimo cha umwagiliaji serikali pia itahakikisha kuwa pembejeo za kilimo, dawa na ruzuku kwa wakulima vinawafikia kwa muda unaotakiwa
Mbegu za mda mfupi na zenye kutoa mazao mengi pia mazao yanayovumilia ukame kama mihogo na mtama yapewe kipau mbele kwa wakulima wa mkoa wa Kilimanjaro ili yaweze kuondoa upungufu wa chakula
Wakulima wengi mkoani hapo hutegemea kilimo cha mvua na wachache sana kutegemea kilimo cha umwagiliaji ambacho hupatikana zaidi katika sehumu za tambarare kwa msaada wa maji yatokayo kwenye misitu mbalimbali kama vile shengena, kindoroko na mlima kamwala na ile yam lima Kilimanjaro
Pia ardhi ya sehemu kubwa ya mkoa huo imechoka sana kutokana na kulimwa kwa mda mrefu bila ya mbolea na hata kuongezeka kwa idadi ya wakazi
Wakati nikiwa Mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Mwanga nilikutana na mzee mmoja aitwae Sawaya Mchwangondo Marisa (85) wa Usangi Vuagha aliweza kunieleza yafuatayo
Historia inaonesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro kila mwaka unaoshia na 4 au kugawanyika kwa nne lazima kuwepo na ukame pamoia na njaa ambayo huathiri sana uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mwaka 1964 Mkoa wa Kilimanjaro ulikumbwa na njaa ambayo wakazi wa mkoa huo hususni wapare waliita njaa ya mkebe kutokana na vyakula vya msaada kupimwa na chombo kiitwacho mkebe
Mnamo mwaka 1968 ilitokea njaa lakini ilikuwa sio njaa kubwa kuliko ile iliotokeo mwaka 1974 ambayo chakula kilichokuwa kinapatikana ni mihongo na yenyewe ilikuwa inapatikana kwa uchache zaidi
Lakini hata hivyo kuanzia mwaka 1978 hali ya chakula ilikuwa sio nzuri ijapokuwa watu wachache wategemeao kilimo peke yake waliathirika zaidi kutokana na mavuno kupatikana lakini yalikuwa kidogo yasiokidhi haja za wakulima
Mwaka 1984 imeelezwa wazi kuwa upungufu wa chakula ulitokea Mkoani Kilimanjaro ulikuwa ni wa kutisha katika kipindi chote ambacho njaa ilshawahi kutokea
Serikali ya mwalim Juliasi Nyerere ulichukua hatua za kuaagiza chakula kutoka nje kilichojulikana kama mahindi ya Yanga(njano) Kwa kipindi hiki Taifa zima lilikuwa na hali mbaya sana ya chakula
Imekuwa kawaida watu wa mkoa huo kuamini kama kila mwaka utakao kuwa unnaishia na nne au nane kwao itakuwa na uhaba wa chakula hivyo mwaka 2008 inafahamika kuwa kutakuwa na upungufu wa chakula
Upungufu wa chakula mkoani Kilimanjaro huwa unasababishwa zaidi na ukosefu wa mvua za uhakika katika kipindi kizima cha mwaka na ukosefu wa elimu ya kuhifadhi chakula
Hata kiwango cha maendeleo kilichofikiwa na Mkoa wa Kilimanjaro kama ujenzi wa nyumba mashule, hoteli na miundo mbinu huwa ni moja ya mambo yanayochangia uharibifu wa mazingira yanayochangia kuchoka kwa aridhi
Kutegemea kilimo cha mkono kwa wananchi wengi mkoani Kilimanjaro ni moja ya sababu zinazofanya kutokea kwa upungufu wa chakula ambao hurudisha nyuma kasi ya maendeleo mkoani hapo.
Wakulima wengi wamekuwa hawatumii mbegu sahihi ambazo hazijahakikiwa na wataalamu kwa ubora hivyo kufanya mkulima kutopata mazao ambayo yangemtosheleza katika maisha yake
Pia sehemu nyingi za mkoa wa Kilimanjaro hawana elimu juu ya programme ya maendeleo ya sekta kilimo yaani ASDP ambayo ingeweza kuwasaidia wakulima wengi na kuwawezesha kuondokana na njaa.
Wananchi wa mkoa huo wanatakiwa kutumia mfuko huo wa ASDP katika kuibua miradi mbalimbali ili aweze kupanua uwigo wa upatikanaji wa chakuala na kufanya maisha kuwa marahisi
Mfano katika vijiji vya kata ya Jipendea ambapo hupata maji kutoka sehemu za milimani ikiwemo Usangi, Ugweno na Kilomeni wangeweza kutumia ile asilimia 75 ya uwekezaji inayotolewa na serikali na wahisani kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji
Upo muhimu wa kuongeza idadi ya mabwanashamba ili kuhakikisha kuwa kilimo kinaendelezwa kiufanisi ili kuepukana na majanga ya njaa
Ijapokuwa kunawafugaji ni wengi mkoani Kilimanjaro lakini wanategemea kilimo zaidi ya ufugaji
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bwana Abrahamani Babu alisema kuwa wafugaji wa mkoa huo wauze baadhi ya mifugo yao ili waweze kununu chakula cha kutosheleza mahitaji yao
Yupo mtaalamu wa mifugo aitwae DR BSJ Msangi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo alisema kuwa changamoto zinazowakumba wafugaji wa Mkoa huo ndizo ambazo kumnyima mfugaji na mkulima kufaidi matunda ya kazi yake na kushindwa kujikomboa na njaa za mara kwa mara
Hata ivyo alisema kuwa upande wa soko la nyama sio taizo ijapokuwa lipo moja la Mgagau ambalo linategemewa na wafugaji wengi wa vijijini na mjini.
Hivyo soko la mifugo ndani ya Mkoa huo sio zuri la kumuwezesha mkulima au mfugaji kuweza kutegemea mifugo ili kuondoa uhaba wa chakula unao wakumba mara kwa mara
Serikali inampango wa kuanzisha namna ya usindikaji wa maziwa ili mfugaji kuweza kupata manufaa kupitia kwenye maziwa na
Lakini ikumbukwe kuwa kuuza mifugo sio suluhisho la kuondoa njaa, kutokana na kuwa gunia moja la mahindi ni kata ya shilingi 280000 na 30000 na bei ya ngombe mmoja ni kati ya laki moja na nusa (150000) na laki mbili (200000) ambapo ni sawa na magunia 5 na magunia 6
Kiasi hicho hakiwezi kuhudumia mahitaji ya familia kama chakula, mavazi,ada ya shule na kujitibu upatapo magonjwa kwa muda wa mwaka mzima
Mifugo inayopatikana mkoa wa Kilimanjaro haiwezi kuondoa njaa kutokana uhaba, na udhaifu wa mifugo yenyewe
Ukame unapo tokea sehemu husababisha Mazao ya chakula kuwa na bei ya juu, mazao mengine ka mifugo yanashuka bei kutokana na ukosefu wa pesa na malisho kwa mifugo
Kwani ukame husababisha mifugo kufa au kukosa afya hivyo kuuzwa kwa bei ya chini ili kukwepa kuwapoteza kabisa
Hivyo ukame unapotokea sehemu Fulani ,mifugo haiwezi kuondoa njaa kwa sababu hata yenyewe huwa inaathirika na ukame na hivyo soko lake linapungua
Hata hivyo wafugaji wengi wa mkoa wa Kilimanjaro hawajawezeshwa kufuga il kupata manufaa ya mifugo yao lakini wao hufuga kama sehemu ya utamaduni wao
Mifugo yao mingi haipatiwi chanjo za magonjwa na hawana elimu ya ufugaji wa kitaalamu ambao ungewawezesha kupata manufaa ya ufugaji
Ili wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro uondokane na njaa za mara kwa mara mbali ya kushiriki kilimo cha umwagiliaji wanatakiwa kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa ili kupata mitaji na kuboresha mifugo yao ikiwa ni pamoja nakupata chanjo za mifugo yao
Mkoa wa Kilimanjaro ni mojawapo ya Mikoa ambayo ina wasomi wengi kuliko Mikoa mingine wataalamu hawa wanatakiwa kushirikiana na kuwashauri na kutoa utaalamu wao ili kuondoa tatizo hili ambalo limekuwa likijirudia kila mara
Katika Tarafa ya Usangi Mkoani Kilimanjaro msimu wa maharage huvunwa kwa kiasi kikubwa lakini wakulima huyauza, tena kwa gharama ndogo, hivyo Serikali za Mitaa zisimamie uuzaji wa mazao ya chakula kiholela ili kuhifadhi chakula cha akiba
Monday, November 2, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment