Monday, November 2, 2009

UCHAGUZI WA MWAKA 2010 NA KIWANGO CHA ELIMU

Uchaguzi wa 2010 na elimu

Katika uchaguzi wa mwaka 2010 utakuwa wa kipekee kuliko chaguzi zote ambazo zimetokea hapa Tanzania kutokana na kulenga wanajua kusoma na kuandika tu.

Kwa dondoo za uchaguzi ujao kwa wale wasiojua kusoma na kuandika hawatapata nafasi ya kuwachagua viongozi wao kwa kuwa fomu za kupigia kura zinamtaka kila mpaga kura kuandika majina ya wagombea wake tofauti na vipindi vilivyopita ambapo watu walikuwa wanaweka alama ya tiki

Hayo yamebainika jana baada ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kata ya Segerea mtaa wa Ugombolwa bibi Mariam Machicha kwa tiketi ya cha cha Mapinduzi CCM alipokuwa anaongea na wanachama wakati wa kampeni za chama chake

Alisema utaratibu huu wa kuandika majina ya wagombea katika kupiga kura umetoka ofisi ya Waziri mkuu TAMISEMI kwa makubaliano ya vyama vyote vya siasa hivyo hauwezi kubadilika kwa urahisi

Ni wazi kuwa utaratibu huu unawatenga watanzania wasiojua kusoma na kuandika kupata nafasi ya kutumia haki yao ya msingi ya kumchagua wamtakaye

Hata hivyo inaonekana kuwa elimu imechukua nafasi yake kwani kutokana na jamiii kuwa imeelimika kwa kiasi kikubwa inawapasa wagombea wenyewe wawe ni wenye elimu ili kukabiliana na changamoto zilizopo

No comments:

Post a Comment